Na.Issack Gerald-Mpanda,Katavi Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh. William Tate Ole Nasha,amemwagiza Mrajishi wa vyama vya ushirika Tanzania,kuhakikisha anaunda timu ya ukaguzi ndani ya Siku 14 ili kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku katika chama cha msingi cha ushirika cha Mpanda Kati kilichopo Wilayani Mpanda. Wa-tatu kutoka kushoto aliyeshika kifuani mwake ni Naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa Wilaya ya Mpanda Muda mfupi kabla ya kuanza kikao na wakulima Chama cha Msingi Mpanda Katati,aliyevaa kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima na wengine katika picha ni wakuu wa idara Wilayani Mpanda ...