WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA,MMOJA KUTISHIA KUUWA KWA MANENO MWINGINE KUUZA KIWANJA KWA ZAIDI YA MTU MMOJA
Na.Issack Gerald-Mpanda
MTU mmoja amefikishwa katika mahakama
ya Mwanzo mjini Mpanda jana, akikabiliwa na shtaka la kuuza kiwanja kwa gharama
ya shilingi laki sita na baadaye kukiuza kwa mtu mwingine.
Imeelezwa mahakamni hapo kuwa,
mshtakiwa Shukuru Salum alitenda kosa hilo tarehe nane mwezi Juni mwaka 2015
katika eneo la Nsemulwa mjini Mpanda kwa kumuuzia Bi Aziza kiwanja na hatimaye
kukuiuza kwa mtu mwingine ambaye tayari ameshajenga katika kiwanja hicho.
Akitoa ushahidi mbele ya hakimu wa
mahakama hiyo Robert Nyando, malamikaji amesema mshtakiwa aliahidi kurejesha
fedha hizo lakini hadi sasa hajatekeleza.
Hakimu Nyando amesema mahakama imeona
mshtakiwa ana kesi ya kujibu na kumtaka ajitetee. Mshtakiwa katika utetezi wake
amesema ana mashahidi wawili ambao ameamuriwa na mahakama kuwapeleka mahakamani
hapo tarehe 1 mwezi Februari mwaka huu, kesi hiyo itakaposikilizwa kwa ajili ya
utetezi.
Wakati huo huo,mtu mmoja amefikishwa
katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda, akikabiliwa na shtaka la kutishia kuua
kwa maneno.
Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu
Robert Nyando, Koplo Fulgenzce wa jeshi la polisi Mpanda amemtaja mshtakiwa
kuwa ni Noel Katobasho (76) na alitenda kosa hilo tarehe tano mwezi huu katika
kijiji cha Uruwila na aliwatishia kuwaua walalamikaji Pascalia Makamba na Gaudence
Katobasho, kuwa wakiendelea kulima katika mashamba anayodai ni mali yake,
wataona atakachowafanyia.
Hakimu Nyando ameamuru mshtakiwa
apewe dhamana ya shilingi laki mbili na mdhamini awe na kitambulisho, na
kuagiza katika kesi hiyo abaki mlalamikaji mmoja na mwingine awe shahidi,
polisi ibadili hati ya mashtaka baada ya kubainika ana shtaka la pili.
Kesi hiyo itatajwa tena terehe mbili
mwezi Februari mwaka huu.
Comments