TFS WASISITIZA KUWATIMUA WANANCHI WANAOVAMIA HIFADHI ZA MISITU-Agosti 23.2017
WAKALA wa huduma za misitu nchini TFS Mkoani Tabora imeendelea kusisitiza azma yake ya kuwaondoa wananchi wote waliovamia kwenye maeneo ya hifadhi kufuatia uharibifu mkubwa unaofanywa na wananchi hao kutokana na kuendesha shughuli mbalimbali za kibinadamu ambazo zimekuwa zikichangia uharibifu.