WANAFUNZI 417 WAKATISHA ELIMU WILAYANI MLELE-Septemba 27,2017
Na.Issack Gerald-Mlele Katavi ZAIDI ya wanafunzi 417 wa sekondari katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamekatisha masomo yao kwa kipindi cha kati ya mwaka 2014 na 2016 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba na utoro Hali hiyo imebainishwa na Afisa elimu idara ya Sekondari Bw.Sylivanus Raphael Kunambi ambapo amesema kuwepo changamoto ya wanafunzi kuikatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro na mimba. Kunambi amesema kwa mwaka 2014 wanafunzi 108 sawa na asilimia 17.4 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa katika mwaka huo hawakuhitimu huku mwaka 2015 idadi ya wanafunzi ambao hawakumaliza masomo yao ikiongezeka na kufikia 160 sawa na asilimia 22.9 wakati huo kwa mwaka 2016 wanafunzi 149 sawa na asilimia 20 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa wakishindwa kuhitimu elimu ya sekonadri.. Aidha ametaja sababu nyingine inayosababisha wanafunzi kutohitimu elimu ya Sekondari ni pamoja na jamii ya wafugaji wanaohama hama katika wilaya ya Mlele hal...