SERIKALI YAOMBWA KUWAANGALIA UPYA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR
Mkurugenzi Umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar Asia Abuu Salami ameiomba serikali na Taasisi mbalimbali za maendeleo nchini,kuwapa kipaumbele zaidi watu wenye ulemavu na wasiojiweza pindi zinapotokea fursa za kimaendeleo kwa wananchi. Amesema ni vyema Watu wenye ulemavu kupewa haki sawa za kimaendeleo na watu wengine wasokuwa na ulemavu ili kila mmoja wao ajihisi huru kama wengine kwani nao wakiwezeshwa wanaweza. Aidha Mkurugenzi Asia amebainisha kuwa bado watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi katika jamiii ikiwemo ukosefu wa vifaa wanavyotumia kwa shughuli zao za kila siku kama vigari vya kutembelea,Fimbo,Miwani na kadhalika. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Hassan Hatibu Hassan amewashauri watu wenye ulemavu Mkoani humo kuanzisha Jumuiya ya pamoja itakayowawezesha kurahisisha upatikanaji wa mahitaji yao. Habari zaidi ni P5TA...