TCCIA KATAVI : SERIKALI ITAFUTE MFUMO WA KUDUMU KUSIMAMIA SEKTA YA KILIMO,MENEJA MPANDA KATI NAYE ASEMA UZALISHAJI WA TUMBAKU UMEPUNGUA KUTOKA KILO 3.5 - 1.4 MILIONI
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi CHAMA cha watu wenye kilimo,viwanda na Biashara TCCIA Mkoani Katavi,kimeishauri serikali kutafuta mfumo wa kudumu utakaosimamia sekta ya kilimo ikiwemo kusimamia mfumo wa usambazaji wa pembejeo za kilimo hapa nchini ili wakulima walime kilimo chenye tija kwao kutokana na matumizi sahihi ya pembejeo hizo ikiwa zitaletwa kwa wakati.