MAADHIMISHO YA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI BADO KIZUNGUMKUTI
Na.Issack Gerald Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi (SHIVYAWATA)limesema mpaka sasa hawana uhakika wa kufanya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani kwa sababu ya uhaba wa pesa. Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bw.Issack Mlela wakati akizungumzia maandaliza ya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu inayaotarajiwa kuadhimishwa Desemba 3 mwaka huu. Kwa upande wake Katibu wa chama cha watu wenye ulemavu mkoani Katavi Bw.Godfrey Sadara pamoja na kuitaka jamii kuwafichua watu wenye ulemavu waliofichwa majumbani pia amesema unyanyapaa unaoendelea dhidi ya kundi hilo linatakiwa kukemewa na kila mmoja. Asasi ya kiraia ya IFI inayohusika na masuala ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi kupitia kwa mratibu wake Raphael Fortunatus imesema bado serikali ni kama imesahau makundi ya watu wenye ulemavu katika kuwawezesha ili wafanye maadhimisho. Zaidi ya shilingi milioni moja inatakiwa ili kufanikisha maadhimisho ya watu we...