WANANCHI MKOANI KATAVI WAMEZUNGUMZIA SIKU YA UKIMWI DUNIANI
Na.Issack Gerald
Baadhi ya wananchi mkoani katavi wamesema ni vyema jamii kubadili
tabia ikiwemo kuachana na ngono zembe ili kuweza kuepukana na maambukizi ya
virusi vya ukimwi.
Mapema leo hii wamebainisha hali hiyo wakati wakizungumzia namna wanavyoielewa siku ya ukimwi duniani ambapo wananchi hao akiwemo Mwajuma Idd Bakary na Islam Said wamesema elimu kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi wamekuwa wakiipata na wameweza kuwahamasisha wengine kupima afya zao.
Sanjari na hayo pia wamewaasa vijana kuhakikisha wanapima afya zao
mara kwa mara na kuwa mabalozi kwa wengine namna ya kujiepusha na maambukizi
mapya ya Ukimwi.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye maambukizi makubwa ya
ugonjwa Ukimwi ambapo kwa miaka ya hivi karibuni Mkoa wa Katavi una asilimia
5.9.
Siku ya ukimwi duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 ya kila
mwaka na kauli mbiu kwa mwaka huu inasema
“Changia
mfuko wa maisha,Tanzania bila Ukimwi inawezekana”
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments