TANZANIA NA KAMPUNI YA BARRICK WAFIKIA MWAFAKA SUALA LA MADINI
Majadiliano kati ya Tanzania na timu ya wawakilishi wa kampuni ya Barrick Gold inayomiliki migodi ya madini hapa nchini,yamekamilika na makubaliano kati ya pande hizo yametiwa saini leo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli Ikulu,Jijini Dar es Salaam. Timu ya Barrick Gold Corporation ilikuwa imeongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo Prof.John Thornton wakati timu iliyowakilisha Serikali ya Tanzania imeongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi. Miongoni mwa mambo waliyokubaliana ni kutekeleza mwelekeo mpya wa biashara ya madini ambapo kutakuwa na mgawanyo sawa wa faida ( yaani Tanzania kupata asilimia 50 na Barrick Gold Corporation kupata asilimia 50 ya faida ) na kuundwa kwa kampuni ya ubia wa usimamizi wa migodi ya madini iliyopo Tanzania ambayo itakuwa na makao makuu yake Mwanza na ofisi ndogo Dar es Salaam nchini Tanzania badala ya nchini Uingereza. Mengine ni kufunga ofisi za uhasibu n...