MANISPAA YA MPANDA YATOA ELIMU KWA WATU WENYE ULEMAVU
Na.Issack Gerald-Katavi
HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi imeendesha semina kwa watu wenye ulemavu,ili kuwaelekeza njia
sahihi wanazotakiwa kutumia ili kukidhi vigezo vya kupewa mikopo kwa ajili ya
kufanya shughuli za maendeleo.
Katika semina hiyo,Afisa maendeleo ya
jamii Manispaa ya Mpanda Linus Kalindo,amewataka watu wenye ulemavu Manispaa ya
Mpanda kuainisha shughuli wanazoweza kuzifanya kwa ufasaha ili mikopo
watakayopewa iwe chachu ya maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA)Mkoani Katavi Issack
Mlela,amewataka watu wenye ulemavu kupuuza maneno yanayowakatisha tamaa kuwa watu
wenye ulemavu hawawezi kufanya shughuli za maendeleo.
Makundi ya watu wenye ulemavu ambayo
yameshiriki katika semina hiyo ambayo imefanyikia shule ya msingi Azimio, imewashirikisha
watu wenye ulemavu wa kutoona,kutosikia, viungo na wenye ulemavu wa ngozi aulibino.
Julius Kipeta,Prasida Kameme na
Godfrey Sadara Pamoja na mamb mengine wametaka haki zao za msingi hasa mambo
yanayogusa suala uchumi zizingatiwe ili kutoendelea katika lindi la umaskini.
Afisa maendeleo ya Jamii Manispaa ya
Mpanda Bw.Linus Kalindo kusema kuwa kuna mifutko mitatu ya vijana,wanawake
ambayo ni ya kitaifa pia amesema kuna mfuko wa wajasiliamali katika wilaya ya
Mpanda.
Wakati huo huo ameahidi kufuatilia katika bajeti ya Halmshauri ya
Manispaa ya Mpanda ili kujua kiasi cha fedha walichotengewa watu wenye ulemavu
kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuwa hata mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu alisema katika mgawanyo wa asilimia 10 za
mapato ya ndani ya halmshauri,vijana hupata 4%,wanawake 4% na watu wenye
ulemavu 2%.
Kikao kingine kitakachowaelimisha
watu wenye ulemavu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuunda vikundi
kinatarajiwa kufanyika wiki ijayo kikishirikisha watalaamu wa Halmshauri ya
Manispaa ya Mpanda na makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu.
Kwa mjibu wa sheria namba 9 ya mwaka
2010 iliyopitishwa na bunge la Jamhuri ya Muunano wa Tanzania mwaka
2010,inaitaka serikali na jamii,kutoa haki sawa katika kila Nyanja kama
elimu,afya na huduma nyingine za kibinadamu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments