Dkt Roselyn Akombe Kwamboka alizaliwa 1976 katika kaunti ya Nyamira , na kusomea katika chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuelekea nchini Marekani kwa masomo zaidi. Anamiliki shahada ya uzamifu katika maswala ya sayansi na kimataifa mbali na shahada nyengine kama hiyo katika somo hilo kutoka chuo kikuu cha Rutgers . Hadi uteuzi wake katika tume hiyo alifanya kazi kama katibu katika Umoja wa Mataifa mjini New York, wadhfa ambao anasema ulimwezesha kuwa na uzoefu katika maswala ya uchaguzi duniani. Uwezo wake mkuu alisema mbele ya kamati ya bunge nchini Kenya , ni kutatua migogoro na kwamba ameishi ng'ambo kwa takriban miaka 15, hatua iliomwezesha kuelewa zaidi mahitaji ya watu wanaoshi ughaibuni wakati wa uchaguzi. Kwamboka alielezea kwamba alichukua uamuzi huo kama Mkenya mzalendo aliyetaka kulihudumia taifa lake. Alichukua likizo katika Umoja wa Mataifa hatua inayomaanisha kwamba hatopokea hata shilingi kutoka Umoja wa mataifa wakati ambapo amekuwa akiifanyia kazi IEBC....