Posts

Showing posts from January 21, 2016

TAMISEMI YAAGIZWA KUSIMAMIA VIZURI HALMASHAURI

Na.Issack Gerald-Katavi WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndiyo kitovu cha nchi na kwamba kila Mtanzania ameelekeza jicho lake pale kwa sababu anasubiri kupata huduma ya msingi.

MAAFISA ELIMU NSIMBO WAPEWA SIKU 6 KUHAKIKISHA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUINGIA SEKONDARI WANARIPOTI

Na.Agness Mnubi-Nsimbo. MAAFISA elimu sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo wamepewa siku 6 kuanzia jana, kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanaripoti.

JAMII NSIMBO YAOMBWA KUSHIRIKI MATENGENEZO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Na.Vumilia Abel-Nsimbo JAMII wilayani Nsimbo mkoani katavi imeombwa kushiriki katika matengenezo madogo madogo ya miundombinu ya barabara.

MKOA WA KATAVI KUTOA SEMINA KWA VIONGOZI WA NGAZI ZA MITAA ILI KUTAMBUA MAJUKUMU YAO

Na.Boniface Mpagape:Mpanda SERIKALI Mkoani katavi inatarajia kutoa semina kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi za vijiji, kata na tarafa ili watambue vyema majukumu yao.

WACHIMBAJI DHAHABU ZAIDI YA 200 MPANDA WAPIGWA MARUFUKU UCHIMBAJI,VITENDO VYA WIZI VYAIBUKA

Na.Issack Gerald-Mpanda Wachimbaji   wadogowadogo wa dhahabu katika mgodi wa Kampuni Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesikitishwa na kitendo cha serikali kuwapiga marufuku uchimbaji wa madini katika mgodi huo kwa madai kuwa eneo hilo ni miliki ya makambi ya jeshi.

WANAFUNZI WANYESHEWA MVUA WAKISOMEA CHINI YA MIEMBE WILAYANI MPANDA,WAZAZI WAISHIWA NGUVU WAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Sambwe iliyopo mtaa wa Kampuni   Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda,wameiomba serikali kuwasaidia kumalizia ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ili wanafunzi hao waondokane na adhaa ya kunyeshewa na mvua   inayoambatana na radi wakiwa chini ya miembe.                                                          Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Sambwe wanavyoonekana katika picha katika madarsa yaliyokuwa yakitumika mwezi septemba mwaka jana ambao hata hivyo miti hiyo unayoiona hakuna mti hata mmoja wanasomea chini ya mwembe                                     ...