WACHIMBAJI DHAHABU ZAIDI YA 200 MPANDA WAPIGWA MARUFUKU UCHIMBAJI,VITENDO VYA WIZI VYAIBUKA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu katika mgodi wa
Kampuni Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesikitishwa na kitendo cha serikali
kuwapiga marufuku uchimbaji wa madini katika mgodi huo kwa madai kuwa eneo hilo
ni miliki ya makambi ya jeshi.
Hayo yamebainishwa na wachimbaji hao
wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
Sambamba na Mpanda Radio mgodini hapo
kuhusu namna wanavyoathirika kutokana na kufukuzwa katika mgodi huo.
Wamesema kuwa wanategemea mgodi huo
kuendesha maisha ya kila siku ikiwemo kusomesha watoto na kulipia kodi ya
nyumba.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kampuni
Bw.Simon James amesema kuwa,kufukuzwa kwa wachimbaji hao wapatao 200 kumepelekea
vitendo vya wizi kuibuka ambapo jana mifugo ikiwemo nguruwe na mbuzi kadhaa wameibwa
katika makazi ya watu.
Kwa mjibu wa maelezo ya wajimbaji hao
walioanza kuchimba eneo hilo miaka ya 1980 wamesema kuwa wanategemea kuendesha
maisha kutokana na mgodi huo.
Baadhi ya wachimbaji wadogo ambao
wamezungumzia khusu wanavyoathiliwa na kufukuzwa katika mgodi huo ni pamoja na
Athman Omary,Lucas Juma,Nuru Hassan na Faustin Method Kamatasimba
Kwa upande wake Mjumbe wa seriklai ya
Mtaa wa Kampuni Bi.Flora Simon Mpenda,amesema kuwa kufukuzwa kwa wachimbaji hao
kumeathiri mapato ya kuendesha shule ya Msingi Sambwe.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Mpanda Bw.Wilium Philipo Mbogo amesema kuwa suala hili lipo katika mamlaka husika kwa mazungumzo ili lipatiwe ufumbuzi.
Wiki iliyopita,madiwani wa balaza la Manispaa ya Mpanda kupitia kikao chake cha januari 14 mwaka huu waliiomba Manispaa ya Mpanda kuweka mipaka kati ya eneo la jeshi na makazi ya raia ili kuondoa migogoro ya ardhi.
Wiki iliyopita,madiwani wa balaza la Manispaa ya Mpanda kupitia kikao chake cha januari 14 mwaka huu waliiomba Manispaa ya Mpanda kuweka mipaka kati ya eneo la jeshi na makazi ya raia ili kuondoa migogoro ya ardhi.
Comments