RAIS MAGUFULI AMTEUA MNADHIMU WA JWTZ APANDISHA VYEO MABRIGEDIA 10 KUWA MAJENERALI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Rais wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli Pamoja na uteuzi huo,Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali. Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu ya Rais,Gerson Msigwa Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu. Aidha,Mhe.Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao; 1. Brig Jen. J.G. Kingu 2. ...