MATUMIZI YA TOCHI BARABARANI MKOANI KATAVI ZATAJWA KUPUNGUZA AJALI KWA MWAKA 2017
Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoani Katavi limesema kuwepo kwa tochi za kudhibiti mwendokasi kumesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali za barabarani. Hatua hiyo imebainishwa na Askari wa kitengo cha Usalama Barabarani John Shindika wakati hali ya usalama katika kipindi cha mwaka 2017. Aidha Shindika amewataka watumiaji wa barabara kuwa makini wawapo barabarani ili kujiepusha na ajali zisizo za lazima. Katika hatua nyingine Shindika amesema suala la kuzuia ajali ni wajibu wa kila mtu hivyo kila mmoja yampasa kuzuia ajali kwa namna yoyote Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED