MTOTO MCHANGA WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI AOKOTWA NA WATOTO AKIWA AMETELEKEZWA NA MAMA YAKE
Na.Issack Gerald Mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya mwezi mmoja mpaka mitatu Wilayani Mpanda Mkoani Katavi ameokotwa akiwa ametelekezwa na mama yake mzazi ambaye hata hivyo hajatambulika. Kuokotwa kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike kumethibitishwa na Afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bi.Redigunga Mayorwa ambaye amesema mtoto huyo ameokotwa na w atoto waliokuwa wakicheza katika mtaa wa Airtel kata ya uwanja wa Ndege. Bi.Mayorwa amesema watoto waliomuokota akiwa amefunikwa majani ambapo walimpeleka kwa wazazi wao na hatimaye wazazi hao kumpeleka mtoto katika kituo cha polisi Wilayani Mpanda . Kwa mjibu wa Bi.Mayorwa mpaka sasa mtoto aliyeokotwa Desemba 1 mwaka huu akiwa hana majeraha wala tatizo lolote la kiafya,yupo katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa uangalizi maalumu na anaendelea na afya njema. Ametoa wito kwa mama wa mtoto huyo kufika hosptali ya Manispaa ya Mpanda kumchukua ili ampatie malezi yanayostahili. Tukio hilo linatokea ik...