UHABA WA VYUMBA VYA MADARSA MKOANI KIGOMA WANAFUNZI ZAIDI YA 2000 WAKOSA KUJIUNGA NA SEKONDARI.
Upungufu wa vyumba vya madarasa wilayani Uvinza Mkoani Kigoma imekuwa sababu ya zaidi ya wanafunzi 2000 kukosa nafasi ya kujiunga na masomoa ya sekondari kwa mwaka 2018. Kutokana na hali hiyo,imewalazimu wakazi wa kijiji cha Nyanganga wilayani humo kuamua kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ili wanafunzi waliochaguliwa waanze masomo. Wilaya hiyo ina upungufu wa vyumba vya madaras 73 ambapo hata hivyo wanafunzi wengi wanalzamika kusafiri umbali wa karibu masaa 3 kutoka nyumbani kufuata shule katika vijiji vya jirani na wengine kulazimika kuhama nyumbani kuishi karibu na shule hizo. Kama sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo, Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dk.Fustine amechangia mifuko 20 ya saruji na kuwataka wananchi kushirikiana katika miradi mbambali ya maendeleo yao. Nao Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bw.MwanamvuaMlindo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Weja Ngolo wametoa pamoja na kusema kuwa wameweka m...