Posts

Showing posts from April 11, 2018

RAIS MAGUFULI AMTEUA MWENYEKITI WA BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU (NBAA)

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Isaya Jayambo Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Kwa mjibu wa Taarifa iliyotolewa leo na katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Jairo unaanza leo tarehe 11 Aprili,2018. Prof.Jairo ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com