Posts

Showing posts from January 28, 2018

HABARI PICHA MKOANI KATAVI WAKATI WA UFUNGUZI WA WIKI YA SHERIA

Image
Askari katika maandamano ya ufunguzi wiki ya Sheria Tanzania Mkoani Katavi katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) Katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Muhando na Mkuu wa Wilaya Mpanda Lilian Charles Matinga wakati wa ufunguzi wa wiki ya sheria Tanzania Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Watumishi wa mahakama wakishikilia bango wakiwa sambamba na wanafunzi katika Manispaa ya Mpanda wakati wa ufunguzi wa wiki ya Sheria Tanzania Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Wanafunzi wa shule mkoani Katavi wakishiriki maandamano katika uzinduzi wa wiki ya sheria Tanzania Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Watumishi wa mahakanma katika maandamano ya uzinduzi wiki ya sheria Tanzania Mkoani Katavi (PICHA NA.Issack Gerald) Bango wakati wa ufunguzi wa wiki ya sheria Tanzania Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald)

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MAHAKAMA KUPATA HAKI

Image
Wananchi Mkoa wa Katavi wametakiwa kujenga tabia ya kuitumia mahakama kama Chombo cha kupatia haki kama kichocheo cha kuimarisha dhana ya Utawala bora  hapa Nchini. Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Muhando wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria  ambayo imeanza kuadhimishwa katika Viwanja vya mahakama ya  wilaya Mpanda. Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama mkoani Katavi,MH Ommary Hassani Kingwele amesema dhima kubwa ya uwepo wa wiki ya elimu ya sheria ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata uelewa wa sheria. Madhimisho hayo ya sheria mwaka huu yaliyo na kauli mbiu ‘’ matumizi ya tehama katika utoaji haki kwa wakati na kwa kuzingatia maadili ’’ kilele chake kitakuwa Februari moja mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi meja jenerali mstaafu Rafael Muhuga. H...

MAHAKAMA YA RUFAA YAWAKANA CHADEMA

Image
Mahakama ya Rufaa imesema hakuna rufaa ya uchaguzi wa Jimbo la Longido iliyopo mahakamani hapo. Mahakama hiyo imetoa kauli hiyo wakati Chadema ikiilalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu kufanyika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo kwa madai kwamba kuna kesi mahakamani hapo. Uchaguzi huo mdogo ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Longido kwa tiketi ya Chadema Onesmo ole Nangole ushindi wake kutenguliwa na Mahakama Kuu. Mara kadhaa Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe na Ole Nangole wamekaririwa na vyombo vya habari wakidai kuna rufaa katika Mahakama ya Rufani. Viongozi hao wamekuwa wakiilalamikia NEC kuwa iliendesha uchaguzi mdogo katika jimbo hilo wakati rufaa ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomvua ubunge Ole Nangole ikiwa haijatolewa uamuzi. Hata hivyo,Mahakama ya Rufaa imesema uchaguzi mdogo uliofanyika Longido ulikuwa halali kwa kuwa hakuna rufaa yoyote iliyoko mahakamani hapo. Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa,Elizabeth Mkwizu amesema hakuna ruf...

ACT- WAZALENDO KUZUNGUKA MIKOA 5 UKIWEMO KATAVI

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Ndugu Dorothy Semu,anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mikoa mitano ya Tanzania Bara akiambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho. Ziara hiyo ya siku nane itaanza tarehe 30 Januari 2018 hadi Februari 6, 2018 kwenye mikoa ya Kahama ambao ni Mkoa Maalum wa Kichama,Kigoma,Katavi,Shinyanga,Tabora na Kigoma. Aidha taarifa ya Chama hicho imebainisha kuwa katibu ataambatana na Ndg.Wilson Mshumbusi ambaye ni Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee Taifa,Ndg.Janeth Rithe ambaye ni Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa pamoja na Katibu wa Sera na Utafiti Ndg.Idrisa Kweweta. Moja ya majukumu ambayo Dorothy Semu atayafanya ni kukagua uhai wa Chama,kutoa maelekezo ya ujenzi wa chama, kusikiliza Kero na changamoto za wanachama na kuzipatia ufumbuzi. Mbali na hayo Katibu Mkuu huyo pia atakagua maendeleo ya zoezi la uchaguzi wa ndani ya chama huku ikielezwa kuwa ziara hiyo pia itawalenga wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo wa maeneo hayo. Habari za...