Posts

Showing posts from January 30, 2018

WABUNGE WAPYA CCM WALA KIAPO BUNGENI

Image
Mkutano wa 10 wa Bunge umeanza leo mjini Dodoma kwa wabunge wapya watatu wa CCM kula kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika,Dk Tulia Ackson. Wakati wabunge hao wakila kiapo,takribani wabunge 50 wa upinzani walikuwa nje ya ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria. Walioapishwa ni Dk Damas Ndumbaro (Songea Mjini), Justin Monko (Singida Kaskazini)  na Dk Stephen Kisurwa wa Longido. Pia,Dk Tulia aliomba wabunge kusimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama ambaye alifariki dunia Novemba mwaka jana. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MWENYEKITI WA BUNGE AKATISHA KUSOMWA MAONI YA UPINZANI

Image
Msemaji wa upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria,Ally Salehe amesusa kusoma maoni ya upinzani ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali baada ya Mwenyekiti wa Bunge,Andrew Chenge kukataa kusomwa kwa baadhi ya maneno yaliyomo katika maoni hayo. Salehe alikuwa akisoma maoni hayo leo Januari 30 mwaka 2018 kwa niaba ya msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria,Tundu Lissu aliyeko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi Novemba 7 mwaka jana. Maneno yaliyozuiwa na Chenge kusomwa na upinzani ni kuhusu matukio ya uhalifu nchini, likiwemo la kushambuliwa kwa Lissu. Salehe alianza kusoma maneno hayo lakini alipofika aya ya nne alikatizwa na Chenge akimtaka asubiri, baadaye kumueleza kuwa lugha iliyotumika katika ukurasa kwa kwanza na pili wa hotuba hiyo si ya kibunge. Baada ya kauli hiyo,Salehe amesema upinzani unaiamini na unaisimamia hotuba hiyo kwa kuwa wabunge wote wanayo nakala yake,akaomba kuiwasilisha na kurejea kuketi. Habari zaidi ni P5TANZANIA ...

RAILA ODINGA AJIAPISHA KUWA ‘RAIS WA WANANCHI WA KENYA’

Image
Kiongozi  wa upinzani Raila Odinga (NASA) ameapishwa kuwa ‘Rais wa Wananchi’ wa Kenya licha ya kugomea uchaguzi mkuu wa marudio nchini humo. Raila Odinga amefika  leo katika Uwanja wa Uhuru Park pamoja na viongozi wengine wakuu wa NASA akiwemo Moses Wetangula na Musalia Mudavadi na kujiapisha akishika Biblia. Aidha, mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa Chama Cha Wiper hakuwepo wakati wa kuapishwa kutokana na kuhofia kukamatwa, ambapo Odinga amesema ataapishwa baadaye. “Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya, hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya, maelekezo mengine mtayapata baadae,” alisema Odinga baada ya kuapishwa. Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ‘ si mapinduzi ya serikali’ Raila aligomea uchaguzi huo kwa sababu za kusema kuwa tume ya Uchaguzi nchini humo si ya Uhuru na haki. Uchaguzi huo wa marudio ulikuja baada ya Mahakama ikiongozwa na Jaji Maraga kutengua Uchaguzi wa awa...

NECTA WATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017

Image
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba. Katibu Mtendaji wa Necta,Dk Charles Msonde Jumla ya watahiniwa  385,767 walisoailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017,kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06. Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30,2018 Katibu Mtendaji wa Necta,Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09. Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo,watapata fursa hiyo mwaka huu. Dk.Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani  matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu. Shule 10 bora 1. St. Francis Girls ya Mbeya 2.Feza Boys ya ...