Posts

Showing posts from March 11, 2018

RAIS MAGUFULI ASEMA ANAPATA TABU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Pombe Magufuli amekiri kupata wakati mgumu katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri kutokana na kuwa Mkoa wa Singida kujaa Wabunge wenye sifa zote za kushika nyadhifa hizo . Akiwa katika uzinduzi wa kiwanda cha mafuta ya alizeti mkoani  Singida,Rais Magufuli amesema kwamba anafurahishwa sana na utendaji kazi wa wabunge hao kiasi kwamba alitamani kuwateua wote kuwa katika baraza lake. Rais amesema kwamba Wabunge wa mkoa huo wamekuwa wakimfurahisha katika utendaji kazi wao wa kuwatumikia wananchi. Aidha Rais Magufuli amekiri kufurahishwa na wakazi wa Singida kwani wamekuwa wakitekeleza kauli ya 'Hapa Kazi Tu' kwa vitendo kwa  kulima sehemu kubwa ya mkoa huo ambapo amejionea mwenyewe akiwa katika safari ya gari kuelekea mkoani hapo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

BARAZA LA WAKUNGA LATOA TAMKO

Image
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limelaani na kutoa pole kwa Wauguzi kutokana na matukio yaliyofanywa na viongozi ikiwemo kuwekwa rumande na kupigwa katika mazingira yao ya kazi. Taarifa kutoka katika baraza hilo,iliyotolewa na Lena   Mfalila imesema vitendo hivyo ni udhalilishaji na ni kinyume cha miongozo ya kisheria inayosimamia ushughulikiaji wa tuhuma za uvunjifu wa nidhamu na sheria wakati wa kazi.

RAIS JOHN MAGUFULI ATOA AGIZO KWA WAZIRI WA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kuhakikisha wamiliki wa viwanda vya ndani wanaajiri wazawa. Ametoa agizo hilo leo Jumapili Machi 11,2018 wakati akizindua kiwanda cha kufua vyuma cha Kahama Oil Mill mjini Kahama mkoani Shinyanga.

TUNDU LISSU KUFANYIWA UPASUAJI WA GOTI

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Tundu Lissu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine wa goti la kulia Machi 14,2018 katika Hospitali ya Chuo kikuu cha Leuven, Gasthuisberg ili kumnusuru asipatikane na athari za mifupa kutojiunga kwa wakati.

JESHI LA POLISI LAWAZUIA ACT-WAZALENDO KUFANYA MIKUTANO

Image
Jeshi la Polisi wilayani Mvomero Mkoani Morogoro limekitaka chama cha ACT Wazalendo wilayani humo kusitisha kufanya mikutano ya ndani.

WAZIRI ATOA AGIZO KWA IGP DHIDI YA WATAKAOANDAMANA

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya. Mwigulu ametoa hiyo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli aliyopo Mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo leo hii (Machi 11, 2018) amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika maandamano hayo ni namna ya watu wanatawanywa ili kusudi waje kulalamika kuwa serikali ndio imeuwa watu wake.