Posts

Showing posts from April 20, 2018

WANANCHI NSIMBO WAOMBA KUBORESHEWA HUDUMA YA MAJI DIWANI AKATAA KUWEKA WAZI MIPANGO

Wananchi wa kijiji cha Mtakuja kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameiomba serikali kushughulikia miundombinu ya huduma ya maji kijijini hapo ili wananchi waondokane na tatizo la kutofanya shughuli za maendeleo kwa sababu ya kupoteza muda mrefu wkifuatilia maji. Wamesema serikali imekuwa ikisema itaongeza mabomba ya maji ambapo mpaka sasa hakuna mipango inayotekelezwa kadri siku zinavyosonga mbele licha ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Nsimbo na Diwani wa kata hiyo kutoa ahadi. Mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja Daud Peter Nyasio amekiri hali ya huduma ya maji katika kijiji hicho kuwa mbaya ambapom amesema visima viwili vilivyopo havikidhi idadi ya wananchi zaidi ya elfu tatu wa kijiji hicho wanaotakiwa kuapa maji. Hata hivyo Reward Sichone ambaye Diwani wa Kata ya Kapalala inayojumuisha vijiji vya Mtakuja,Songambele na Kapalala ameiambia Mpanda Radio kuwa hana jambo lolote la kuzungumza na chombo cha habari kuhusu suala la maji katika kata ya Kapal...

ACT-WAZALENDO KATAVI WATOA MAAZIMIO MIGOGORO YA ARDHI KATAVI

Chama cha ACT-Wazalendo mkoani Katavi kimeazimia kuishinikiza serikali kuchukua hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi inayowakabili  wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi. Joseph Mona ambaye ni Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Katavi akizungumza katika mkutano wa chama hicho amesema kikao hicho kilichofanyika jana kililenga kufanya tahimini ya namna ambavyo serikali ya mkoa inavyoshughurikia migogoro ya ardhi inayoendelea kufukuta. Mona ametaja baadhi ya kero za wananchi zimetokana na serikali kuchukua baadhi ya maeneo yaliyokuwa makazi ya wananchi kwa madai kuwa maeneo hayo   yalikuwa katika hifadhi za misitu. Aidha Mona ametaja baadhi ya maeneo yenye migogoro kuwa ni pamoja na vijiji vya Litapunga,Luhafwe,Sitalike,Ugalla, Kanoge na Mpanda Ndogo. Hivi karibuni Chama cha ACT-Wazalendo wakiwa wameambatana na viongozi wa kijiji cha Sitalike pamoja na wananchi wa kijiji cha Sitalike walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu R...