JUMAMOSI KUU
Jumamosi kuu ni siku ya Juma kuu inayoadhimisha hasa pumziko la mwili wa Yesu Kristo kaburini kabla ya kufufuka kwa utukufu usiku wa kuamkia Jumapili ya Pasaka . Tarehe yake inabadilikabadilika kila mwaka na hata mwaka uleule ni tofauti katika madhehebu ya Ukristo , hasa yanayofuata mapokeo ya mashariki na yale yanayofuata mapokeo ya magharibi . Siku hiyo Misa na sakramenti mbalimbali haziadhimishwi kwa kuwa wafuasi wa Yesu wanatulia kimya wakitafakari matukio ya Ijumaa kuu na kujiandaa washangilie ufufuko wake kuanzia kesha la Pasaka hadi Jumapili ya Pentekoste siku 50 baadaye. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com