JUMAMOSI KUU
Jumamosi
kuu ni siku ya Juma kuu inayoadhimisha
hasa pumziko la mwili wa Yesu Kristo kaburini kabla
ya kufufuka kwa utukufu usiku wa
kuamkia Jumapili ya Pasaka.
Tarehe yake
inabadilikabadilika kila mwaka na hata mwaka uleule ni tofauti katika madhehebu ya Ukristo,
hasa yanayofuata mapokeo ya mashariki na yale yanayofuata mapokeo
ya magharibi.
Siku
hiyo Misa na sakramenti mbalimbali
haziadhimishwi kwa kuwa wafuasi wa Yesu wanatulia kimya wakitafakari
matukio ya Ijumaa kuu na kujiandaa washangilie ufufukowake
kuanzia kesha la
Pasaka hadi Jumapili ya Pentekoste siku 50 baadaye.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments