TAMKO LA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI KESHO MACHI 24
# Kifua Kikuu(TB) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani. # Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua Kifua Kikuu kila mwaka Duniani na Milioni Moja kati ya hao ni watoto wenye umri chini ya miaka 15. # Tafiti nyingi zinaonesha kuwa karibia theluthi moja ya Watanzania tayari wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu na wanaishi na vimelea mwilini mwao. # Kauli mbiu ya mwaka huu inasema *” Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB.”* #Nchini Tanzania kila mwaka jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu. # Nitoe wito kwa viongozi wa ngazi zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele. # Napenda kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa zake zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo vya Umma na Binafsi. # Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua Kiku...