Posts

Showing posts from March 21, 2018

SERIKALI YATOA TAHADHARI UGONJWA HATARI WA DENGUE

Image
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue. Mhe.Ummy Mwalimu Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki,Kati na Kusini ECSA leo jijini Dar es salaam. “Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla,kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu.Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo.Wizara inashauri wananchi wasiwe na hofu,bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya tiba"amesema Waziri Ummy. Aidha Waziri Ummy amesema wakati mwingine dalili za ugonjwa huo zinaweza kufanana sana na dalili za malaria hivyo wananchi wanaaswa kwamba,wakipata homa wahakikishe wanapima ili kugundua k...

MEI MOSI KITAIFA KUFANYIKA JIJINI ARUSHA

Image
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda,Biashara,Taasisi za Fedha,Huduma na Ushauri (Tuico),kimeanza maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) mwaka 2018. Akizungumza katika semina ya kuelimisha na kubadilishana uzoefu iliyowashirikisha viongozi wa matawi mbalimbali ya  Tuico mwishoni mwa wiki,jijini Dar es salaam,Mwenyekiti wa Tuico taifa,Sangeze alisema Shirikisho la Vyama vya Huru vya Wafanyakazi nchini (Tucta),limekiteua chama chao kuwa mratibu wa shughuli zote za Mei mosi kwa mwaka huu.

NECTA YABADILI MFUMO MTIHANI DARASA LA SABA

Image
Baraza la Mitihani Tanzania Nacte,limefanya mabadiliko katika mfumo wa kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi . kwa wanafunzi wa darasa la saba nchini. Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Dk Charles Msonde. Mabadiliko hayo yamefanywa jana na Baraza hilo na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Dk Charles Msonde. Ofisa Habari wa Necta,John Nchimbi amesema mabadiliko hayo yametangazwa na Dk.Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MMILIKI WA TIGO,VIGOGO WA UJERMANI NA DENMARK NAO WAJITOKEZA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli amekutana na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom International Services LLC inayomiliki kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Bw.Mauricio Ramos,Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kwa mjibu wa taarifa ya mawasiliano ya ais Ikulu wamezungumza kuhusu uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini.

RAIS AWAAPISHA MABALOZI WAWILI AKIWEMO IGP MSTAAFU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amewaapisha Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi na IGP Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.

WAFANYABIASHARA KATAVI WAREJESHEWA FEDHA ZAO WALIZOTAPELIWA

Image
Katibu wa jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania mkoani Katavi Bw.Robison Thompson Bumela amethibitisha fedha za kurejeshwa kwa wafanyabiashara waliokuwa wakidai kutapeliwa na baadhi ya makambuni yanayouza mashine za kielektronic (EFDs) hapa nchini. Hatu hiyo meithibitisha leo Ofisini kwake wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu hatima ya malalamiko ya wafanyabiasahara waliokuwa wakidai kutapeliwa fedha bila kupata mashine hizo. Aidha Bw.Bumela amesema wafanyabiashara wachache ambao hawajarejeshejewa pesa zao ni waliokuwa wamelipia bila kupewa risiti na hivyo kuleta ugumu katika ushahidi ili kumbana wakala aliyechuku fedha zao.

RAIS MAGUFULI ATEUA MABALOZI WAWILI YUMO IGP MSTAAFU KUAPISHWA HIVI PUNDE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo atawaapisha Mabalozi Wateule wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Rwanda na Urusi.

RAIS MAGUFULI ATENGUA KIGOGO SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA(NHC)

Image
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Blandina Nyoni na kuivunja bodi hiyo.