NECTA YABADILI MFUMO MTIHANI DARASA LA SABA
Baraza
la Mitihani Tanzania Nacte,limefanya mabadiliko katika mfumo wa kufanya
mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi .
kwa
wanafunzi wa darasa la saba nchini.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Dk Charles Msonde. |
Ofisa
Habari wa Necta,John Nchimbi amesema mabadiliko hayo yametangazwa na Dk.Msonde
katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma.
Nchimbi
amesema katika muundo huo mpya kila somo litakuwa na maswali 45 ambapo kati ya
hayo,maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yatakuwa ya
kujieleza/kuonyesha njia na jibu.
Amesema
katika maswali 40,kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila
swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yakijibiwa kwenye OMR
FORM huku maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.
Kutokana
na muundo huo mpya,Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi
kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments