RAIS MAGUFULI ATEUA MABALOZI WAWILI YUMO IGP MSTAAFU KUAPISHWA HIVI PUNDE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli leo atawaapisha Mabalozi Wateule wawili aliowateua kuiwakilisha
Tanzania katika nchi za Rwanda na Urusi.
Rais Magufuli akiwa na IGP Mstaafu Ernes Jumbe Mangu |
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi imeeleza kuwa Mhe.Rais Magufuli atamuapisha IGP-Mstaafu Ernest
Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.
Aidha amesema Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco
Mumwi ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.
Hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi Wateule hao inatarajia
kufanyika hivi punde kuanzia majiara ya saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Uteuzi huo ulifanyika jana Machi 20,2018
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments