NYUMBA ILIYOTEKETEA KWA MOTO JUZI ,CHUMBA CHA MPANGAJI HASARA NI ZAIDI YA MILIONI MOJA NA LAKI TANO(1,500,000).
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda Imebainika kuwa janga la moto lililotokea juzi katika Mtaa wa Mpadeco Kata ya Mkananyagio Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,umesababisha Bi.Grace Emmanuel Mkazi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio kupata hasara ya Zaidi ya Shilingi Miloni moja na laki tano (1,500 ,000). B.Grace amesema Moto huo uliozuka mchana uliunguza Vitanda 2 vyenye thamani ya laki tano na elfu sitini(560,000),Magodoro mawili 5 kwa 6 yenye thamani ya Shilingi laki tatu(300,000),Maguni ya Mpunga 4 thamani yake zaidi ya Shilingi laki 2(200,000),Upotevu wa fedha taslimu Shilingi laki nne na nusu za mkopo zilizopotea wakati wa uokozi na nguo ambazo tahamani yake haijafahamika. Akizungumza akiwa nyumbani kwake muda mfupi baada ya kutoka hospitali ya Wilaya ya Mpanda,alikolazwa baada ya kuzimia kutokana mshtuko alioupata baada ya kupata hasara hiyo,amesema kuwa hata hivyo hajatambua kiasi alichotumia kwa ajili ya matibabu. Hata hivyo amekwishafungua jarada Polisi ili ili kufany...