ZAIDI YA SHILINGI MIL.9 ZATUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE KATAVI
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) Mratibu wa Mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Fortunatus Raphael amesema mradio huo unaosimamiwa na shirika la IFI,umetumia zaidi ya shilingi milioni 9 kukarabati miundombinu ya shule za msingi Nyerere,Shanwe na Kivukoni katika kipindi cha mwaka 2017/2018. Raphael amebainisha hayo katika taarifa yake kwa wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda,kupitia kikao ambacho kimefanyika katika Ofisi za mradi huo mjini Mpanda. Aidha Raphael amesema Mradi umetoa msaada wa mafuta maalumu kwa ajili ya watu wenye ualbino 44 wakiwemo 25 wa Manispaa ya Mpanda na 19 Halmashauri ya Nsimbo pamoja na kugawa mavazi pia baiskeli kwa watu wenye ulemavu wa viungo. Amesema muda wowote wanatarajia kuwahudumia watoto wenye ulemavu kwa mkoa...