MKUU WA SHULE AJINYONGA OFISINI KWAKE AKIMTAJA MKURUGENZI
MKUU wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter Rubonya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake mapema leo asubuhi. Akielezea tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika shuleni hapo saa 12:30 asubuhi ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne masomo ya ziada baada ya kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika aligundua kuwa hana chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili awape wananfunzi. Amesema baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na mmoja wa wazazi walifika ofisini hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini lakini baada ya kugonga mlango hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini. Mwalim Isaac amesema Mwalimu aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii na mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kiku...