UYOGA WAUA MWINGINE KATAVI
Mtu mwingine mkazi wa kijiji cha Sitalike wilayani Mpanda Mkoani Katavi amefariki
dunia akiwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akipatiwa matibabu na hivyo kufikisha idadi ya watu watatu waliofariki kutokana na kula uyoga
unaosadikiwa kuwa na sumu.
Mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw.Christopher Anjero amemtaja mwanamke aliyefariki leo kuwa ni Mariana
Gerald Sanane ambaye ni Mama wa marehemu wawili waliofariki siku ya jana.
Waliofariki jana kutokana na kula uyoga huo ni Frenki Mayaga ambaye alifariki akipatiwa huduma ya kwanza
katika kijiji cha Stalike huku Erizabeth
George ambaye alikimbizwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akiaga dunia baada ya
kufikishwa katika mlango wa Daktari.
Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambaye alitakiwa kueleza
zaidi kuhusu suala hilo amekana kuzungumza kwa madai ya kutokuwa msemaji kwa
sasa.
Kisa hicho ambacho kimeacha
simanzi kwa jamii kutokana na vifo vya watu watatu wa familia moja kinatajwa
kuwa ni kuwa cha kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments