Posts

Showing posts from December 22, 2017

BUNDI GANI AMEENDELEA KUTANDA KUHUSIANA NA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS?TUMEPOROMOKA TENA VIWANGO VYA FIFA MPAKA NAFASI YA 147 KUTOKA 142

Image
Taifa Stars Tanzania imezidi kudidimia katika viwango vya soka duniani baada ya kushuka kwa nafasi 5 zaidi kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mwezi Novemba. Kupitia taarifa iliyotolewa ljana na Shirikisho la soka duniani FIFA inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka  142 mwezi Oktoba ikiwa imeporomoka kwa nafasi tano kutoka juu. Kwa Uganda wa Afrika Mashariki na Kati,Uganda imeendelea kuongoza ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani huku Senegal ikiwa inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 kwenye viwango hivyo vya FIFA. Kwa upande wa 10 bora,Ujerumani imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Brazil,Ureno,Argentina,Ubelgiji,Hispania,Poland, Uswisi,Ufaransa na Chile. Tanzania ilifanya vibaya kwenye michuano ya CECAFA nchini Kenya mapema mwezi huu pia kwa mwezi Novemba ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Benin. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

UCHUNGUZI MAUAJI YA KIMBARI NCHINI RWANDA UMEKAMILIKA

Image
Majaji wa Ufaransa wamemaliza upelelezi juu ya shambulio la kombora ambalo lilisababisha kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Image caption Rais wa Rwanda,Paul Kagame Ofisi ya mwendesha mashitaka sasa wataamua ikiwa waipeleke kesi mbele ya mahakama ambapo Majaji wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na rais wa sasa wa Rwanda Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba rais wa wakati huo wa taifa hilo Juvenal Habyarimana. Rwanda nayo inawalaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya kimbari huku Upelelezi ukisababisha sintofahamu kati ya mataifa haya mawili kiasi cha Rwanda kuvunja uhusiano wa kidplomasia na ufaransa mwaka 2006. Hata hivyo Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulirejeshwa miaka mitatu iliyopita. Chanzo:bbc Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

NCHINI SUDANI KUSINI MKATABA WA KUSITISHA MAPIGANO KUANZIA SIKU YA KRISMASI WASAINIWA

Image
Image caption Rais wa Sudan kusin,Salva Kiir Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi wameweka saini ya kusitisha mapigano kuanzia siku ya krismasi hatua ambayo imechukuliwa kama kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa miaka minne. Makubaliano hayo yametiwa saini katika mji mkuu wa Ethiopia,Addis Ababa katika mkutano ulioitishwa na IGAD. Makuabliano hayo yanaruhusu makundi ya kutoa misaada kuwafikia wananchi waliobanwa katika maeneo ya mapigano ambapo Mara kadhaa makubaliano ya kusitisha vita yametiwa saini Sudan kusini lakini yote hayakutekelezwa. Maelfu wamepoteza maisha na mamilioni kuyakimbia makazi yao kutokana na machafuko nchini Sudani kusini taifa ambalo lilipata uhuru miaka sita iliyopita. Chanzo:bbc Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MAREKANI KUUTAMBUA JERUSALEM KUWA MJI MKUU WA ISRAEL UN WAPIGA KURA KUPINGA

Image
Image caption Umoja wa mataifa kupinga maamuzi ya Trump Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa umepiga Kura ya kutoyatambua maamuzi ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Makubaliano hayo ya mkutano wa umoja wa mataifa yamefikiwa pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump aliyetishia kuzikatia msaada wa kifedha nchi zote zitakazopinga msimamo wake. Mataifa 120 wameyapigiakura maazimio,baadhi ya mataifa hayo yakiwamo washirika wa karibu wa marekani yaani Japan, Uingereza na Ujerumani yamepiga kura. Canada na Mexico ni moja ya mataifa thelathini na tano ambayo hayakuhudhuria mkutano huo na Wapalestina wameiita hatua ya Umoja wa mataifa kuwa ni ushindi wa Palestina ingawa Israel imeyakataa matokeo. Kabla ya kura,balozi wa marekani katika umoja wa mataifa,Bi Nikki Haley alionya kuwa Marekani haitasahau au kusamehe pale nchi zilizoipinga Marekani zitakapokuja kuomba misaada. Chanzo:bbc Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED