MAREKANI KUUTAMBUA JERUSALEM KUWA MJI MKUU WA ISRAEL UN WAPIGA KURA KUPINGA
Mkutano mkuu wa Umoja
wa mataifa umepiga Kura ya kutoyatambua maamuzi ya Marekani ya kuutambua
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Makubaliano hayo ya mkutano wa umoja wa mataifa
yamefikiwa pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump aliyetishia kuzikatia
msaada wa kifedha nchi zote zitakazopinga msimamo wake.
Mataifa 120 wameyapigiakura maazimio,baadhi ya
mataifa hayo yakiwamo washirika wa karibu wa marekani yaani Japan, Uingereza na
Ujerumani yamepiga kura.
Canada na Mexico ni moja ya mataifa thelathini
na tano ambayo hayakuhudhuria mkutano huo na Wapalestina wameiita hatua ya
Umoja wa mataifa kuwa ni ushindi wa Palestina ingawa Israel imeyakataa matokeo.
Kabla ya kura,balozi wa marekani katika umoja
wa mataifa,Bi Nikki Haley alionya kuwa Marekani haitasahau au kusamehe pale
nchi zilizoipinga Marekani zitakapokuja kuomba misaada.
Chanzo:bbc
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments