Posts

Showing posts from April 5, 2018

RAIS KUZINDUA UKUTA WA MIGODI YA TANZANITE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli kesho Aprili 6,2018 anatarajia kuzindua ukuta wa machimbo ya madini wa Mirerani mkoani Manyara. Hayo yamesemwa leo na Msemaji Mkuu wa jeshi hilo,Kanali Ramadhan Dogoli wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu Upanga-Dar es Salaam.

JWTZ WAONYA WANAOJIHUSISHA NA UTAPELI WA AJIRA JESHINI

Image
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewaonya wote wanaojihusisha na utapeli wa ajira jeshini ambapo limesema litaendelea kuchukulia hatua kali zaidi. Hayo yamesemwa leo na Msemaji Mkuu wa jeshi hilo,Kanali Ramadhan Dogoli wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu Upanga-Dar es Salaam.

MUIGIZAJI MAARUFU NCHINI INDIA,SALMAN KHAN AHUKUMIWA JELA MIAKA MITANO

Image
Muigizaji mkongwe nchini India, Salman Khan amehukumiwa kwenda jela miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuua wanyama jamii ya swala miaka 20 iliyopita.

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMA ZA RAMBIRAMBI WALIOFARIKI AJALI YA BASI LA CITY BOY,ATOA MAAGIZO

Image
Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya basi la kampuni ya City Boy iliyotokea jana Aprili 4,2018. Katika ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Makomero Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora imesababisha vifo vya watu 12 na wengine 46 kujeruhiwa. Ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo lililokuwa limebeba abiria kutoka Karagwe Mkoa wa Kagera kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso la lori lililokuwa likitokea Singida kuelekea Igunga. Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Aprili 5,2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli   mbali na kutoa pole,amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha,kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali. Rais amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri kufikisha salamu zake   za pole kwa wafiwa wote   na amewa...

MKUU WA MKOA ASIKITISHWA WATOTO KUTORIPOTI SEKONDARI

Image
Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amesikitishwa na wazazi ambao hawajawapeleka shuleni watoto wao kujiunga na masomo ya sekondari kidato cha kwanza mwaka 2018 baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2017. Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi ametoa masikitiko yake wakati akifungua vikao vya wadau wa elimu  Mkoani Katavi vikao ambavyo vinalenga kujadili,kutathimini  na kuchukua hatua dhidi ya vikwazo vinavyosababisha Mkoa wa Katavi kufanya vibaya katika ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka 2017 ukishuka kutoka nafasi 3 za juu kitaifa na kufikia nafasi ya 9. Aidha Muhuga amesema mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu,wanafunzi wapatao 240 wilayani Tanganyika walikuwa hawajaripoti shuleni ambapo amewataka madiwani wawahamasishe katika kata zao wawapeleke shuleni watoto wao hata kama hana sare na utaratibu mwingine utaendelea baadaye kubainisha chanzo cha kukosa sare. Aidha Mkuu wa Mkoa katika kupunguza changamoto ya uhaba wa miu...

MAJAMBAZI YAVAMIA NA KUPORA SADAKA KANISANI

Image
Majambazi wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam na kupora fedha na baadhi ya vifaa vya kuendeshea misa usiku wa kuamkia leo. Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango,Uchumi na Fedha wa parokia hiyo,Arnold Kimanganu amesema majambazi hao waliwapiga walinzi kabla ya kuingia kanisani. Paroko wa parokia hiyo,Sunil Kishor amesema majambazi hao walivamia kanisa hilo saa tisa usiku na wameiba fedha na baadhi ya vifaa vya kuendesha misa. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lazaro Mambosasa amekiri kutokea kwa tuki hilo japo amesema hajapata taarifa ya kimaandishi ofisini kwake. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

BASI NA FUSO ZAUA 12 NA KUJERUHI

Image
Watu 12 wamefariki dunia na wengine 46 kujeruhiwa baada ya basi la abiria la City Boy kugongana uso kwa uso na fuso usiku wa kuamkia leo,Aprili 05, 2018  k atika kijiji cha makomelo wilayani Igunga mkoani TABORA Basi la City Boy lilikuwa likifanya safari yake kutoka Karagwe kwenda Dar es Salaam na imetokea baada ya kudaiwa dereva wa fuso kutaka kukwepa shimo na kujikuta fuso hilo likimshinda hivyo  kupelekea kugongana uso kwa uso Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora,Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na tayari majeruhi wamepelekwa hospitali. Hata hivyo,jeshi la polisi limeahidi kutoa taarifa zaidi leo baadaye ikiwemo na hali ya majeruhi wa ajali hiyo. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com