MAJAMBAZI YAVAMIA NA KUPORA SADAKA KANISANI
Majambazi wamevamia Kanisa Katoliki
Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam
na kupora fedha na baadhi ya vifaa vya kuendeshea misa usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango,Uchumi na Fedha wa parokia hiyo,Arnold Kimanganu amesema majambazi hao waliwapiga walinzi kabla ya kuingia kanisani.
Paroko wa parokia hiyo,Sunil Kishor
amesema majambazi hao walivamia kanisa hilo saa tisa usiku na wameiba fedha na
baadhi ya vifaa vya kuendesha misa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam,Lazaro Mambosasa amekiri kutokea kwa tuki hilo japo amesema hajapata
taarifa ya kimaandishi ofisini kwake.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments