BASI NA FUSO ZAUA 12 NA KUJERUHI
Watu 12 wamefariki dunia na wengine
46 kujeruhiwa baada ya basi la abiria la City Boy kugongana uso kwa uso na fuso
usiku wa kuamkia leo,Aprili 05, 2018 katika kijiji cha makomelo wilayani Igunga mkoani TABORA
Basi la City Boy lilikuwa likifanya
safari yake kutoka Karagwe kwenda Dar es Salaam na imetokea baada ya kudaiwa
dereva wa fuso kutaka kukwepa shimo na kujikuta fuso hilo likimshinda hivyo kupelekea kugongana uso kwa uso
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora,Wilbrod
Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na tayari majeruhi wamepelekwa
hospitali.
Hata hivyo,jeshi la polisi limeahidi
kutoa taarifa zaidi leo baadaye ikiwemo na hali ya majeruhi wa ajali hiyo.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments