JWTZ WAONYA WANAOJIHUSISHA NA UTAPELI WA AJIRA JESHINI
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewaonya wote wanaojihusisha na
utapeli wa ajira jeshini ambapo limesema litaendelea kuchukulia hatua kali
zaidi.
Hayo
yamesemwa leo na Msemaji Mkuu wa jeshi hilo,Kanali Ramadhan Dogoli wakati
akizungumza na waandishi wa habari makao makuu Upanga-Dar es Salaam.
Amesema
kuwa kuna baadhi ya majangili hujifanya kuwa ni watumishi wa jeshi hilo na
kuwatapeli wananchi na hivyo wananchi wametakiwa kuwa makini.
Aidha Dogoli amesema askari ambao wamekuwa wakiwabaini
wamekuwa wakiwapatia adhabu ndogo ya kuwafukuza kazi na wengine wanafikishwa
mahakamani.
Kumekuwa kukiripotiwa matukio ya wananchi kutapeliwa
na watu wanajifanya kuwa ni watumishi wa jeshi wakisema wanawatafutia nafasi za
ajira jeshini ambapo mwishoni imekuwa tofauti.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments