Posts

Showing posts from February 2, 2018

RAIS MAGUFULI AMSAIDIA MLEMAVU BAJAJI

Image
Rais waJamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kumsaidia Bajaj Mlemavu wa viungo Bw.Yusuf Abdulrahaman Ndemanga. Bw.Ndemanga amekabidhiwa Bajaji hiyo na Katibu wa Rais Bw.Ngusa Samike,Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Februari 02. Mhe.Rais Magufuli alikutanana Bw.Ndemanga tarehe 25 Agosti,2017 katika sehemu ya abiria wakati akisubiri kupanda kivuko cha MV Magogoni kuelekea Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mara baada ya kukutana na Mhe.Rais Magufuli,Bw. Ndemanga alimuomba msaada wakupatiwa Bajaj ili imsadie kupata kipato. Akikabidhi msaada huo Bw.Ngusa Samike amemtaka Bw. Ndemanga kuitumia Bajaj hiyo vizuri na kujiongezea kipato kitakacho msaidia yeye na familia yake. Kwa upande wake Bw.Ndemanga aliyeongozana na Mkewe Bi.Hawa Mohamed amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa msaada huo na ameahidi kuwa ataitumia Bajaj hiyo vizuri kuzalisha kipato kwa ajili ya familia yake. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI KUWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA WA JWTZ

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kesho anatarajia kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kwa mjibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais I kulu Gerson Msigwa kamisheni hizo atazitunuku katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam. Watakaotunukiwa kamisheni ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi marafiki waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha. Tukio hilo linatarajia kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari hapa nchini kuanzia saa 3:00 asubuhi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

TUNDU LISSU NAYE AMLILIA MZEE KINGUNGE

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu amezungumzia kifo cha Kingunge Ngombale Mwiru akisema historia itamkumbuka. Akizungumza leo Februari 2, 2018  ameanza kwa kusema “namtakia mapumziko mema.” Amesema Mzee Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wenye historia kubwa na alionyesha ujasiri mkubwa wa kuhama chama chake cha CCM bila kuhofia kuhudhuriwa kutokana na mazingira yalivyokuwa. Kingunge aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba nane,Oktoba 4,2015 alitangaza kukihama chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote lakini mara kadhaa alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi aliyekuwa mgombea urais wa Chadema/Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015. Tundu Lissu ambaye ni Rais  wa chama cha wanasheria nchini TLS anapatiwa matibabu nchini ubelgiji baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka uliopita. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA MZUNGUKO WA PILI KUANZA KESHO

Image
Ligi kuu soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena hapo kesho kwa mzunguko wa pili kupigwa katika viwanja mbali mbali. Singida United inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 27 nyuma ya mabingwa watetezi Yanga SC wenye pointi 28 inajipanga kuingia katika mzunguko wa pili hapo kesho siku ya Jumamosi kwa kuivaa Mwadui FC majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Namfua. Michezo mingine itakayo pigwa hapo kesho ni Azam FC waliyo nafasi ya pili kwa kujikusanyia alama 30 katika duru la kwanza itakuwa nyumbani dhidi ya Ndanda FC mechi itakayopigwa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam. Lipuli FC ya Iringa itakuwa na kibarua kizito nyumbani kwake itakapocheza dhidi ya Yanga SC iliyo maliza mzunguko wa kwanza kwa kuwa na pointi 28 ikiwa nafasi ya tatu mtanange utakaopigwa dimba la Samora, wakati Stand United ikiivaa Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Tanzania Prisons iliyo na alama 21 ikiwa nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi wata wakar...

RAIS MAGUFULI AMLILIA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli,amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa na mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru. Kifo cha Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kilichotokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 10:30 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa wake nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam 22 Desemba 22 mwaka jana. Mhe.Rais Magufuli amesema Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye alitoa mchango mkubwa katika juhudi za kupigania uhuru na baada ya kupata uhuru akiwa mtumishi mtiifu wa Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) na katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali. Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu kufuatia msiba huu,Mhe.Rais Magufuli amewapa pole wanafamilia wote,wanachama wa CCM,ndugu,jamaa, marafiki na wote walioguswa na...

MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE AFARIKI DUNIA

Image
Mwanasiasa mkongwe hapa nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru(87) amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na mtoto wa marehemu Kinje Kingunge,amesema baba yake amefariki usiku wa kuamkia leo majira ya saa tisa. Kwa mjibu wa taarifa zilizokuwa zimetolewa mwezi uliopita Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam mwezi mmoja uliopita. Rais Magufuli alimjulia hali Mzee Kingunge alipolazwa hospitalini Mke wa Kingunge Peras Ngombale mwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi Januari kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo. Mzee Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za awamu nne zilizopita na amewa...

MAREKANI YAPATWA WASIWASI NA KENYA

Image
Marekani imeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya matukio yanayotokea nchini Kenya,ambako kiongozi wa Upinzani Raila Odinga alijiapisha mwenyewe kuwa ''Rais wa Wananchi'' siku ya Jumanne. Haki miliki ya picha EPA Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Kenya akijiapisha kuwa ''Rais wa Wananchi'' Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hearther Nauerth amesema malalamiko kuhusiana na uchaghuzi nchini Kenya yanapaswa kusuluhishwa kupitia utaratibu unaofaa wa kisheria. Ameikosoa pia serikali kwa uamuzi wake wa kuvifungia vituo vitatu vya serikali,ambavyo vilijaribu kurusha matangazo ya moja kwa moja tukio hilo la kujiapisha kwa Raila Odinga. Chanzo:bbc Swahili Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED