RAIS MAGUFULI AMSAIDIA MLEMAVU BAJAJI
Rais waJamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kumsaidia Bajaj Mlemavu wa viungo Bw.Yusuf Abdulrahaman Ndemanga.
Bw.Ndemanga
amekabidhiwa Bajaji hiyo na Katibu wa Rais Bw.Ngusa Samike,Ikulu Jijini Dar es
Salaam leo Februari 02.
Mhe.Rais
Magufuli alikutanana Bw.Ndemanga tarehe 25 Agosti,2017 katika sehemu ya abiria
wakati akisubiri kupanda kivuko cha MV Magogoni kuelekea Kigamboni Jijini Dar
es Salaam.
Mara
baada ya kukutana na Mhe.Rais Magufuli,Bw. Ndemanga alimuomba msaada wakupatiwa
Bajaj ili imsadie kupata kipato.
Akikabidhi
msaada huo Bw.Ngusa Samike amemtaka Bw. Ndemanga kuitumia Bajaj hiyo vizuri na kujiongezea
kipato kitakacho msaidia yeye na familia yake.
Kwa
upande wake Bw.Ndemanga aliyeongozana na Mkewe Bi.Hawa Mohamed amemshukuru
Mhe.Rais Magufuli kwa msaada huo na ameahidi kuwa ataitumia Bajaj hiyo vizuri
kuzalisha kipato kwa ajili ya familia yake.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments