MAGUFULI ATEUA MWANASHERIA MKUU MPYA WA SERIKALI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John
Pombe Magufuli amemteua Dokta Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa
serikali.
REUTERS
Kabla
ya uteuzi huo Dokta Kilangi,alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Agustino,kituo cha Arusha na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti
wa Shughili za mkondo wa juu ya mafuta-PURA.
Wakati
huohuo,Rais Magufuli amemteua Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa
serikali.
Kabla
ya uteuzi huo alikuwa Paul Ngwembe,Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania.
Kufuatia
uteuzi huo,Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali
George Mcheche Masaju na Aliyekuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali Gerson
Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama kuu.
Uteuzi
huo pia umeanza jana Februari mosi.
Jana Rais Dkt.John Magufuli
alisema bado kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na
AG (Mwanasheria Mkuu),na ndiyo maana muda mwingine inawapelekea kuwapa
changamoto kubwa Majaji.
Hata hivyo rais kupitia kilele
cha jana cha maadhimisho ya wiki ya sheria Tanzania aliwatuhumu Waziri wa
Katiba na Sheria,Prof.Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa serikali,George
Masaju na kudai kuwa wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na
kutofanyia kazi mambo ya msingi.
Kwa mjibu wa taarifa hiyo ambayo imetolewa na katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi inaeleza kuwa walioteuliwa wanatarajiwa kuapishwa kesho Februari 3,2018
Kwa mjibu wa taarifa hiyo ambayo imetolewa na katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi inaeleza kuwa walioteuliwa wanatarajiwa kuapishwa kesho Februari 3,2018
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments