Posts

Showing posts from September 16, 2017

NDOA ZA JINSIA MOJA ZAMFIKISHA MAHAKAMANI-Septemba 16,2017

Image
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Sharifu Issah maarufu kama Zamda Salumu Mkazi wa Manispaa ya Mtwara, amefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa.

MLIPUKO WA KIPINDUPINDU MBEYAWATU 8 WAFARIKI DUNIA 628 WAPATIKANA NA UGONJWA HUO-Septemba 16,2017

Image
DC Wilayani Mbarali Reuben Mfune Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Mh.Reuben Mfune ameagiza bar zote,migahawa,vilabu vya pombe na grocery kufungwa kwa siku zisizojulikana kutokana na ugonjwa wa kipindupindu kuzidi kusambaa wilayani humo.

WAPENZI WA JINSIA MOJA WAKAMATWA ZANZIBAR-Septemba 16,2017

Mamlaka ya kisiwani Zanzibar imewakamata watu 20 wanaotuhumiwa kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja.

UNDENI VIKUNDI FEDHA KWA AJILI YA WATU WENYE ULEAMAVU ZIPO-Septemba 16,2017

SIKU moja baada ya Shirikisho la watu wenye Ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi kuomba watu wenye ulemavu kuwezeshwa ili kujikwamua kimaisha na hatimaye kujenga uchumi wa taifa,halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imewataka watu wenye ulemavu kuunda vikundi vya kijasiliamali ili wapatiwe mikopo.

MKUU WA MKOA RUKWA AWA MBOGO KUHUSU UVUVI HARAMU-Septemba 15,2017

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen ameionya idara ya uvuvi mkoani humo kuacha mzaha katika suala zima la kupambana na wavuvi haramu kwani ikifanya mzaha vizazi vijavyo vitabaki vikiwashuhudia viumbe wa kwenye maji katika picha na mikanda ya video kama katika mataifa Mengine yalivyo. 

SHIVYAWATA WAOMBA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZESHWE ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI-Septemba 15,2017

Image
SHIRIKISHO la vyama vya watu wenye ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi,limesema watu wenye ulemavu mkoani Katavi bado wanahitaji kuwezeshwa zaidi kama makundi mengine yasiyo na ulemavu ili kujikwamua kimaisha na kujenga uchumi wa taifa.

TANZANIA YASHTUSHWA KUHUSISHWA NA KOREA KASKAZINI-Septemba 16,2017

Image
Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini.