BARAZA LA MAASKOFU KUTEMA CHECHE KESHO KUHUSU HALI YA USALAMA WA TANZANIA NA WATU WAKE
Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania viko hatarini. Katika waraka wa ujumbe wa pasaka unaosambaa katika mitandao ya kijamii na kutarajiwa kusomwa kesho katika makanisa mbali mbali ya KKKT nchini Tanzania, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo. Waraka umeyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji,utesaji,kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa,mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi,vitisho, ubambikiziaji wa kesi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi. Waraka umeongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza,kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge,Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa. jumbe huu kutoka baraza la maaskofu wa KKKT umekuja siku chache tu baada...