KAULI YA WAZIRI ISIPOFAFANULIWA VIZURI INAWEZA KUSABABISHA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU SHULENI
Miaka michache baada ya serikali
yenyewe kufuta adhabu ya viboko shuleni,Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dk.Mwigulu
Nchemba,amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa
kuwafundisha maadili mema na na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike.
Waziri Nchemba ametoa kauli hiyo
wakati akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya
Sekondari Lulumba Wilayani Iramba mkoani
Singida ambapo amesema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi
ili kutengeneza hatma ya nchi.
Katika hatua nyingine amesisitiza
kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora
ya ofisi na vyumba vya madarasa.
Mbali na hayo Dk.Nchemba amesema
majengo ya taasisi za serikali yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani
za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.
Imekuwa ikishuhudiwa baadhi ya walimu wakiwachapa wanafunzi mpaka kusababisha majeraha hata baadhi ya walimu hao kufukuzwa kazi,je,kauli ya Waziri Mwigulu inakuwaje?
Chanzo:Eatv/Mpekuzi Blog
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments