MBUNGE CHADEMA MKOANI KATAVI AIBUKA NA HOJA YA KUPATIKANA DIWANI MWINGINE WA KATUMBA
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi kupitia Chadema Rhoda Kunchela amesema kitendo cha kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kutokuwa na diwani ni kuchelewesha maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo. Hayo yamebainishwa leo na Mbunge huyo na kusema kuwa wananchi wanakosa uwakilishi na kushauri uchaguzi ufanyike ili apatakane diwani mwingine. Katika hatua nyingine Mh Kunchela amezungumzia ziara aliyoifanya mwenyekiti wa Bawacha taifa Halima Mdee amabye pia ni mbunge wa jimbo la kawe na kusema ziara hiyo imefanyika mkoani katavi ikilenga kuimarisha uhai wa chama hicho. Diwani aliyekuwa akiongoza kata hiyo Mh Seneta Baraka mwezi Novemba mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kupokea rushwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED