Posts

Showing posts from November 17, 2017

RAIS MAGUFULI AMETOA MSAADA MSIKITINI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa msaada kwa Msikiti wa Noor Mkange, Miono, wilayani ya Chalinze mkoa Mkoa wa Pwani leo. Waumini wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange,Miono,Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani,wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili. Zulia pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilayani Chalinze mkoa wa Pwani. Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli, amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa. Sheikh Nassor mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo amesema,kwa niaba ya waumini wa Msikiti huo wamemshukuru Mhe.Rais kwa kuitikia ombi lao la kupata zulia na kwamba kwa kutimiza ahadi ...

AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUBAKA MTOTO

Image
Mahakama ya  wilaya ya Mpanda mkoani  Katavi imemuhukumu  Willson  John(34) mkazi wa  Kijiji cha Simbwesa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kutumikia jela kifungo cha  maisha  baada  ya kupatikana  na hatia ya kumbaka  mtoto (7)wakati akiwa anaoga bafuni. Hukumu  hiyo ilitolewa jana  na hakimu mkazi mfawidhi  wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga  Tengwa baada ya kuridhika na  ushahidi  uliotolewa na upande wa  mashtaka. Kabla ya kusoma hukumu  hiyo  hakimu  Tengwa alisema  mtu yoyote  anaefanya kitendo  kama  alichofanya mshitakiwa  huyo  anakuwa amefanya  kosa  kinyume  cha kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza  na 2E  cha  sheria namba 131 kidogo  cha...

WANAFUNZI SHULE YA BIBLIA FPCT KATUMBA WAMETEMBELEA KITUO CHA MPANDA RADIO,MENEJA WA KITUO ATOA NENO KWAO

Image
Na.Issack Gerald Wanafunzi 17 walimu 3 wa shule ya biblia FPCT Katumba Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wametembelea kituo cha Mpanda Radio na kueleza kuridhishwa na namna  kinavyosaidia jamii katika masuala mbalimbali ya kijamii. Kutoka Kushoto WA PILI aliyevaa kitambulisho ni Issack Geral,anayefuata aliyeweka mkono mfukoni ni Meneja wa Mpanda Radio Levocatus Msafiri,mwenye shati ya mikono mifupi aliyeshika kifuani ni mkuu wa vipindi Mpanda Radio Edward Mganga na waliobaki ni wanafunzi isipokuwa aliye karibu na Edward kutoka kulia ni Mkuu wa Shule Mch.Elisa Musenda(PICHA NA.Issack Gerald) Mara baada ya kutembelea kituo hiki,Mkuu wa shule ya biblia FPCT Mchungaji Elisha Musenda pamoja na kuipongeza  Mpanda Radio kwa namna inavyohudumia wananchi amesema kuna kila sababu ya kituo hicho kufika mbali zaidi kimatangazo. Kwa upande wake Meneja wa kituo cha Mpanda Radio Bw.Levokatus Msafiri,amesema kituo kitaendelea kushirikiana na kila mwananchi kwa lengo la kuchochea maend...

JELA MIAKA 30 MKOANI RUKWA KWA KOSA LA KUBAKA MTOTO

Image
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30  Jela,kulwa Dase (35) mkazi wa kijiji cha Paramawe wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 15. Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Ramadhan Rugemalila alisema mahakama imeridhishwa pasipo kuacha shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hivyo kumuhukumu mtuhumiwa kifungo hicho. Alisema kufuatana na mwenendo wa kesi hiyo ambapo mashahidi wanne walitoa ushahidi upande wa mashitaka  mtuhumiwa alikutwa na hatia chini ya kifungu cha sheria f namba 130(1) na namba (2)(e) NA 131 sura ya 16 ya kanuni ya  adhabu. Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi Hamimu Gwelo uliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 12 mwaka huu majira ya saa 8 mchana. Aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine baada ya vitendo kama hivyo kukithiri  katika...

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA KITUO CHA AFYA

Image
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqaro ameweka jiwe la msingi katika kituo cha afya kinachojengwa kata ya Mushono halmashauri ya jiji la Arusha ambapo kitakapokamilika kitahudumia wananchi zaidi 20,698 katika eneo hilo. Akizungumza baaada mara baaada ya kuweka jiwe la msingi mkuu  wa Wilaya Fabian  Daqaro amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Magufuli inahakikisha vituo vya  afya vinakuwa karibu na wananchi kupata uduma kirahisi ili kupunguza tatizo la wananchi  kufuata huduma umbali mrefu. Akisoma taarifa kuhusu kituo hicho cha afya Mushono mganga mkuu wa jiji la Arusha Dokta Simon Chacha amesema kuwa kituo hicho kinajengwa kwa awamu mbili awamu ya kwanza ni kujenga msingi na ya pili ni kujenga boma pamoja na kupaua. Kwa upande wa diwani wa kata na wananchi wa Mushono wamesema kuwa wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwasogezea wananchi huduma karibu zaidi na kituo hicho kitakapo kalimika kita wapunguzia adha ya kutembea kwenda mjini...

JESHI LA POLISI LIMEAGIZA UCHUNGUZI WA NDEGE ULIYOUA UFANYIKE

Image
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Mkoani Arusha limeagiza kufanyika uchunguzi kwa ndege ndogo ya aina ya CQ241 ya kampuni ya Coastal iliyo anguka na kusababisha vifo vya watu kumi na moja akiwemo na rubani wa ndege iyo aliye tambulika kwa jina moja la Dewal akiwemo na abiria kumi ambao wanafanyiwa uchunguzi wa utambuzi wa uraiya wao na majina yao.  Kamanda Charles Mkumbo amedhibitisha kutokea kwa ajali iyo jana majira ya saa nne asubui katika eneo Empaakai Creater iliopo katika mamlaka ya ifadhi ya Ngoro Ngoro mkoani arusha wakati ikielekea safarini katika ifadhi ya Setrengeti na ndipo kupoteza mawasiliano na kuanguka chini uku chanzo chake ni kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya . Mkumbo amesema wameagiza jopo la utafiti kuchunguza ajali iyo kwani sio mara ya kwanza kuanguka kwa ndege ya kampuni iyo ya Coastal uku ikiwa imepita miezi miwili kuanguka kwa ndege nyingine ndogo ya kampuni iyo iyo . Amesema jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kufanya taratibu za kuopoa mihili ...

KESI INAYOWAKABILI BAADHI YA MAAFISA WA BENKI YA POSTA TABORA IMEENDELEA KUAHIRISHWA

Image
Kesi Ya Uhujumu Uchumi Inayowakabili Baadhi Ya Maafisa Wa Benki Ya Posta Imeendelea Kuahirishwa Katika Mahakama Ya Hakim Mkazi Mkoa Wa Tabora Baada Ya Upande Wa Jamhuri Kushindwa Kuwasilisha Mahakamani Hapo Hatua Ya Maelezo Iliyofikiwa Ya Upelelezi Wa Shauri Hilo. Mbele Ya Hakim Mkazi wa Mahakama Tabora EMANUEL NGIGWANA Wakili Wa Serikali TITO MWAKALINGA Ameieleza Mahakama Kuwa Anaendelea kufanya Mawasiliano na Mawakili Waliopo Kwenye Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai Nchini DPP Kuhusu Hatua iliyofikiwa ya Upelelezi wa Jalada hilo. Jopo La Mawakili Upande Wa Washitakiwa Wakiongozwa Na Wakili PAULUSI RWEYONGEZA Walitaka Kujua Mahakamani Hapo Kama Shauri Hilo Limetelekezwa Au La Kwa Kuwa Watuhumiwa Wanaendelea Kusota Mahabusu huku wakiwa Wametenganishwa na Familia zao ambazo bado zinaendelea kuwategemea. Akijibu Hoja Hiyo Wakili Upande Wa Jamhuri TITO MWAKALINGA Ameomba Mawakili Waelewe Kuwa Shauri Hilo Bado Linafanyiwa Kazi Kisheria Na Kwamba Ofisi Ya DPP Haijawahi Kuicheze...

UVAMIZI NA UNYANG’ANYI WA PIKIPIKI MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Mtu mmoja anayefahamika kwa jina Korode Merikiolo mkazi wa kata ya Katumba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,amevamiwa usiku wa kuamkia leo na kunyang’anywa pikpiki aliyokuwa akiendesha akitokea soko la Mnyaki huku akishambuliwa na watu wawili ambao hawajatambulika. Bw.Korode Merikiolo pamoja na kusema kuwa alipgwa sehemu mbalimbali za mwili wake,amesema wakati wanatekwa na kunyang’anywa pikipiki alikuwa amembeba Lea Bitabo ambapo msichana huyo amesema wakati akitaka kukimbia alizuiliwa na wanyang’anyi hao. Mwenyekiti wa kijiji cha Mnyaki B Bw.Yusto Zambayembi kwa upande wake amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema alipokea taarifa hizo saa 3 usiku. Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo. Hata hivyo licha ya  matukio ya watu kuvamiwa, kujeruhiwa na kunyang’anywa mali zao kutokea na kuripotiwa katika kituo cha polisi Katumba na wengine kutibiwa katika kituo cha afya Katumba,Kamanda wa POlisi Damasi Ny...