KESI INAYOWAKABILI BAADHI YA MAAFISA WA BENKI YA POSTA TABORA IMEENDELEA KUAHIRISHWA
Kesi Ya Uhujumu Uchumi Inayowakabili Baadhi Ya
Maafisa Wa Benki Ya Posta Imeendelea Kuahirishwa Katika Mahakama Ya Hakim Mkazi
Mkoa Wa Tabora Baada Ya Upande Wa Jamhuri Kushindwa Kuwasilisha Mahakamani Hapo
Hatua Ya Maelezo Iliyofikiwa Ya Upelelezi Wa Shauri Hilo.
Mbele Ya Hakim Mkazi wa Mahakama Tabora
EMANUEL NGIGWANA Wakili Wa Serikali TITO MWAKALINGA Ameieleza Mahakama Kuwa
Anaendelea kufanya Mawasiliano na Mawakili Waliopo Kwenye Ofisi Ya Mkurugenzi
Wa Makosa Ya Jinai Nchini DPP Kuhusu Hatua iliyofikiwa ya Upelelezi wa Jalada
hilo.
Jopo La Mawakili Upande Wa Washitakiwa
Wakiongozwa Na Wakili PAULUSI RWEYONGEZA Walitaka Kujua Mahakamani Hapo Kama
Shauri Hilo Limetelekezwa Au La Kwa Kuwa Watuhumiwa Wanaendelea Kusota Mahabusu
huku wakiwa Wametenganishwa na Familia zao ambazo bado zinaendelea kuwategemea.
Akijibu Hoja Hiyo Wakili Upande Wa Jamhuri
TITO MWAKALINGA Ameomba Mawakili Waelewe Kuwa Shauri Hilo Bado Linafanyiwa Kazi
Kisheria Na Kwamba Ofisi Ya DPP Haijawahi Kuichezea Mahakama kama walivyokuwa
Wamedai.
Kwa Upande Wake Hakim Mfawidhi Wa Mahakama
Hiyo EMANUEL NGINGWANA Amesema Kuwa Ofisi Ya DPP Itimize Majukum yake Kisheria
ili Haki Iweze Kutendeka.
Kesi Ya Uhujumu Uchumi Namba Tatu Ya Mwaka
2017 Inayo Wakabili Watuhumiwa 16 Wakiwemo Baadhi ya Maafisa Wa Benki ya Posta
Imeahirishwa Hadi Novemba 29 Mwaka Huu Itakapo Tajwa Tena.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments