UVAMIZI NA UNYANG’ANYI WA PIKIPIKI MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina
Korode Merikiolo mkazi wa kata ya Katumba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
Mkoani Katavi,amevamiwa usiku wa kuamkia leo na kunyang’anywa pikpiki aliyokuwa
akiendesha akitokea soko la Mnyaki huku akishambuliwa na watu wawili ambao
hawajatambulika.
Bw.Korode Merikiolo pamoja na kusema
kuwa alipgwa sehemu mbalimbali za mwili wake,amesema wakati wanatekwa na
kunyang’anywa pikipiki alikuwa amembeba Lea Bitabo ambapo msichana huyo amesema
wakati akitaka kukimbia alizuiliwa na wanyang’anyi hao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mnyaki B
Bw.Yusto Zambayembi kwa upande wake amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
akisema alipokea taarifa hizo saa 3 usiku.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi
amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo.
Hata hivyo licha ya matukio ya watu kuvamiwa, kujeruhiwa na
kunyang’anywa mali zao kutokea na kuripotiwa katika kituo cha polisi Katumba na
wengine kutibiwa katika kituo cha afya Katumba,Kamanda wa POlisi Damasi Nyanda
amekana kuwa na taarifa za matukio hayo.
Takribani wiki mbili
zilizopita,matukuio ya watu kuvamiwa nyakati za usiku na kuporwa mali zao
yalitokea ambapo moja na tukio ni mmoja wa wakazi kuvamiwa na kuibiwa fedha na
mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja ambapo katika kipindi
hicho matukio yapatayo matatu yameripotiwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments