MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA KITUO CHA AFYA
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqaro
ameweka jiwe la msingi katika kituo cha afya kinachojengwa kata ya Mushono
halmashauri ya jiji la Arusha ambapo kitakapokamilika kitahudumia wananchi zaidi
20,698 katika eneo hilo.
Akizungumza baaada mara baaada ya kuweka jiwe
la msingi mkuu wa Wilaya Fabian Daqaro amesema serikali ya awamu ya
tano chini ya Raisi Magufuli inahakikisha vituo vya afya vinakuwa karibu
na wananchi kupata uduma kirahisi ili kupunguza tatizo la wananchi
kufuata huduma umbali mrefu.
Akisoma taarifa kuhusu kituo hicho cha afya
Mushono mganga mkuu wa jiji la Arusha Dokta Simon Chacha amesema kuwa kituo
hicho kinajengwa kwa awamu mbili awamu ya kwanza ni kujenga msingi na ya pili
ni kujenga boma pamoja na kupaua.
Kwa upande wa diwani wa kata na wananchi wa
Mushono wamesema kuwa wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwasogezea
wananchi huduma karibu zaidi na kituo hicho kitakapo kalimika kita wapunguzia
adha ya kutembea kwenda mjini kiutafuta huduma ya Afya.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Adhuman Kihamia
amesema malengo ya kituo hicho ni kuanza kufanya kazi rasmi mwezi wa sita
lakini ifikapo mwezi wa tatu kitaanza kufanya kazi rasmi kikiwa na maitaji yote
muhimu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments