RAIS MAGUFULI AKUTANA NA UJUMBE WA PAUL KAGAME AAGANA NA BALOZI WA ZIMBABWE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli jana amekutana na Mjumbe Maalum wa Rais wa Rwanda na aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.Donald Kaberuka na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na umoja wa Afrika (AU). Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa Dkt.Kaberuka amesema uchumi wa Tanzania unakua vizuri na amempongeza Mhe.Rais Magufuli kwa jinsi anavyosimamia ukuaji wa uchumi huo. Dkt.Kaberuka amesema katika mazungumzo hayo pia amewasilisha ujumbe wa Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame ambaye kuanzia mwezi huu atakua Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na ndiye aliyekabidhiwa majukumu ya kufanya mabadiliko ndani ya umoja huo. Wakati huo huo,Mhe. Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Zimbabwe hapa nchini anayemaliza muda wake Mhe. Edzai Chimonyo na kumpongeza kwa uwakilishi mzuri alioufanya kwa miaka 10 aliyoiwakilisha Zim...